Lugha


English English
አማርኛ Amharic
العربية Arabic
العربية - الأردن Arabic (Jordanian)
العربية التونسية Arabic (Tunisian)
Armenian Armenian
Sign Language American Sign Language
বাংলা Bengali (India)
भोजपुरी Bhojpuri
Bosanski Bosnian
မြန်မာဘာသာ Burmese
中文(繁體,香港) Cantonese (Traditional)
中文(简体) Chinese (Simplified)
中文(繁體) Chinese (Traditional)
Hrvatski Croatian
Français French
Deutsch German
ગુજરાતી Gujarati
Hausa Hausa
हिन्दी Hindi
Bahasa Indonesia Indonesian
Italiano Italian
日本語 Japanese
ಕನ್ನಡ Kannada
한국어 Korean
Кыргызча Kyrgyz
کوردی Kurdish
ພາສາລາວ Lao
𑒧𑒻𑒟𑒱𑒪𑒲 Maithili
മലയാളം Malayalam
मराठी Marathi
नेपाली Nepali
ଓଡ଼ିଆ Odia
فارسی Persian/Farsi
Polski Polish
Português Portuguese
ਪੰਜਾਬੀ Punjabi
ਪੰਜਾਬੀ (ਪੱਛਮੀ) Punjabi (Western)
Русский Russian
Română Romanian
Slovenščina Slovenian
Soomaali Somali
Español Spanish
Kiswahili Swahili
தமிழ் Tamil
తెలుగు Telugu
ไทย Thai
Türkçe Turkish
اردو Urdu
Tiếng Việt Vietnamese
Yorùbá Yoruba

Mungu Anatumia Watu wa Kawaida


Karibu kwenye mafundisho ya Zúme. Zúme ni neno la Kigiriki linalomaanisha “chachu.”

Yesu anatuambia kwamba Ufalme wa Mungu ni kama mwanamke ambaye alichukua kiasi kidogo cha “ Zúme” na kukiweka kwenye kiasi kikubwa cha unga uliokandwa.

Alipokuwa akichanganya, chachu ilienea hata unga wote ukachachuka.

Yesu alikuwa anatufundisha kwamba mtu wa kawaida anaweza kutumia kitu kidogo sana na kusababisha kishindo kikubwa sana!

Ndoto yetu ni kufanya yale Yesu alisema -- kuwasaidia watu wa kawaida duniani kote kutumia vifaa vidogo kutoa vishindo vikubwa katika Ufalme wa Mungu!
 
Maagizo ya Yesu ya mwisho kwa wanafunzi wake yalikuwa rahisi. Alisema  -- Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi –enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwa batiza kwa jina la baba, na la Mwana, nala Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.

Maagizo ya Yesu yalikuwa rahisi –Mkawafanye Wanafunzi
 
Amri yake jinsi ya kutekeleza hayo ilikuwa rahisi – mkafanye wanafunzi popote muendapo

  • Mkafanye wanafunzi kwa kuwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu
  • Mkawafanye wanafunzi kwa kuwafundisha yote niliyowaamuru

Kwa hivyo ni hatua zipi za kuwafanya wanafunzi?

  • Tunawafanya wanafunzi kila wakati – popote tuendapo na tunapoenda
  • Mtu akifanya uamuzi wa kumfuata Yesu – sharti abatizwe
  • Wanapokua – tufundishe kila mwanafunzi jinsi ya kutii vitu vyote alivyoamuru Yesu.

Kwa vile kitu kimoja alichoamuru ni kufanya wanafunzi, hiyo inamaanisha kila mwanafunzi anayemfuata Yesu anastahili kujifunza jinsi ya kutengeneza wanafunzi pia.

Hao wanafunzi wanastahili kutengeneza wanafunzi. Na hao wanafunzi nao wakatengeneze wanafunzi, pia.

Kuzidisha wanafunzi. Hivyo ndivyo  Zúme inafanya kazi.

Ni kama chachu – ilijichanganya ndani mwa unga uliokandwa hadi wote ukawa chachu.

Wakati Yesu alipotoa amri hii ya kwenda kuwafanya wanafunzi, alitoa ahadi pia.

Yesu alisema – Nitakuwa nanyi daima. Hata ukamilifu wa dahari.

Kila mfuasi wa Yesu anapaswa kuzingatia ahadi ya kuwa Yesu yu pamoja nasi. Kwa sababu Yeye yuko!
 
Lakini pia inamaanisha kila mfuasi wa Yesu anapaswa kujitoa kwa ukweli kwamba Yesu anataka kila mmoja wetu atengeneneze wanafunzi. Kwa sababu Yeye alifanya.
 
Yesu alisema – nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni mkawafanye wanafunzi.
 
Mamlaka ambayo Yesu hutegemea wakati Anatutuma - ni mamlaka Yake
 
Yesu anasema hakuna mamlaka iliyo juu kuliko hiyo. Hakuna utamaduni uliyo na mamlaka zaidi.
 
Hakuna utamaduni uliyo na mamlaka zaidi. Hakuna sheria duniani iliyo na mamlaka zaidi.
 
Yesu alisema – nendeni mkawafanye wanafunzi.
 
Na kama Zúme - chachu – tutaendelea kuenda na kukua hata kazi yote ikamilike.