Utakuwa na uwezo wa kufuata kwenye PDF ya kikao kwa kipindi hiki, lakini tafadhali hakikisha kwamba kila mwanachama wa kundi Lako ana nakala iliyochapishwa ya vifaa kwa ajili ya vikao vya baadaye.
- Unapofikiria kuhusu kanisa, kitu gani huja mawazoni?
- Kuna utofauti gani kati ya picha hiyo na kinachoelezwa kwenye video kama "Kanisa vivi hivi"?
- Unafikiri ni gani ingekuwa rahisi kuzidisha na kwa nini?
- Kwa nini ni muhimu kujifunza na kusikia na kutambua sauti ya Mungu?
- Je, kusikia na kumuitikia Bwana ni kama kupumua? Kwa nini au kwa nini sivyo?
S.O.A.P.S. Kusoma Bibilia
Kusikia kutoka kwa Mungu mara kwa mara ni kipengele muhimu katika uhusiano wetu wa kibinafsi Naye, na katika uwezo wetu wa kuwa watiifu kushiriki katika kile anachofanya karibu nasi.
Makundi ya Uwajibikaji
Biblia inatuambia kwamba kila mfuasi wa Yesu siku moja atawajibika kwa kile tunachofanya na kusema na kufikiria. Makundi ya uwajibikaji ni njia nzuri ya kujiandaa!
Hongera! Umekamilisha Kipindi cha 1.